Ukiachilia mbali suala zima la kutupia ulimi pale kati, mixa ming’aro ya ziada kiasi cha kumpiga jeki yule asiyekuwa na mauzo ya kutosha…. Leo namdondosha kwenu ‘HANDSOME’ ambaye yeye binafsi anaamini anashine bila bling bling kwasababu ana Mwili na Sura nzuri na hii ni tangu enzi za analogi hadi digito (SWAGGA)

Anaitwa Dully sykes au Prince Dully sykes a.k.a Blazameni Dully a.k.a Mr Misifa ambaye ametuibukia pande hizi ili kuturimaindi kuhusu Historia ya huu mziki wetu wa Bongo Flava.

Huyu Blaza alianza Muziki miaka ya 1994 kipindi cha akina Saleh Jabir, naposema kipindi cha akina Salehe Jabir namaanisha ni enzi zile wasanii wetu wanachukua nyimbo za nje na kuzitafsiri kwa kiswahili.. ni kipindi ambacho kilifuata baada ya kile cha ‘MIE NI MSELA/ NINA KICHWA KAMA PERA/SIWEZI KWENDA JELA/ KWASABABU NA MAHELA…’3 Bila shaka hiki ni kipindi ambacho Ubunifu ulikua umeanza kupewa kipaumbele, naam, hii ni hatua ya 3 baada ya ile ya kuimba nyimbo za nje kama zilivyo, kipindi hicho tulikuwa na wakavaji (hawa ni wale ambao walikua wakiipenda ngoma tu lazima waikariri na waifanye kwenye show zao) so tukawa na vikundi vya Naughty by nature  wabongo, Michael Jackson wa bongo, Mc Hammer wa bongo na Vannilla Ice wa Bongo.

Elvis,Michael Jackson,UB 40, ni baadhi ya wale waliomuinspaya(kumvutia kimuziki) huyu Prince wa Bongo Flava.. na alikua akiimba nyimbo zao na kuzicheza kama wao kwenye maafali ya darasa la saba au birthday parties za mitaa yake ya kariakoo, show yake ya kwanza ilipigika ndani ya shule ya Shaaban Robert mnamo mwaka 1996 na huko aliwaambia INFORMER ya SNOW,na Dj alikua P FUNK kutoka shule ya IST (International school of Tanganyika

Dully alipenda kuwa Mwanamuziki mwenye nyimbo zake mwenyewe na sio zile za kuiga,na katika kulikwepa hilo alijitengenezea utaratibu wa kuandika nyimbo kwa kufuata hisia zake yeye mwenyewe kama yeye,kwahiyo hakuwa na jinsi zaidi ya kuibuka maeneo ya studio za  Don Bosco mnamo mwaka 1998.

Hata hivyo juhudi zake za kurekodi nyimbo Don Bosco ziligonga Mwamba baada ya kukuta foleni kubwa pale studio na zile nenda rudi za Maproducer wetu.. ‘waliniambia niwalipe Elfu Tano ili nirekodi..na hiyo ndo ilikua bei kamili ya studio, nikawapa na pia kama haitoshi nikanunua hadi Chrome.. tatizo studio ilikua bize halafu mie nilikua na mizuka ya kutosha so sikutaka kuwapa pointi, inshoti  niliwapotezea lakini hadi leo ile loss ya ELfu Kumi inaniuma.. © Dully

Judgement day(ilirekodiwa Marimba records chini ya Mpishi Mr Chaz) ndo title ya Ngoma yake ya kwanza,kwa bahati mbaya haikufanya vizuri kabisa, hakuna aliyeikubali au kuielewa.. lakini siku zote mwanzo huwa mgumu au vipi? Well,hakuna asiyejua ya kwamba Hustla huwa hachoki kwasababu Nia ya mtu huwa imo ndani ya dhamira yake, so ni yeye wakuitengua au kuitilia mkazo

Dully aliamua kujifanyia research yeye mwenyewe ili akijue kile kilichosababisha Tonge lake lisifike Mdomoni na kabla Udhaifu wake haujamulemea,alibahatika kukutana na Dj Stevie B au ‘SKILLZ’(kitambo hicho alikua anaswagua pale Sugar ray)  desemba ya mwaka 99 na ushauri pekee aliopewa ni ‘UNAIMBA VIZURI TATIZO WABONGO WENGI HAWAJUI KIINGEREZA, NADHANI UTAFIKA HUKO UNAKOTAKA KWENDA KAMA UTATUMIA KISWAHILI KWENYE TUNGO ZAKO MDOGO WANGU’

Unajua ukweli huwa unahitaji maneno machache tu, nadhani ndo maana ikaclick fasta kwenye ubongo wa mwanafleva huyu na kabla ya karne ya 21 kuingia tayari alikua ashakutana na Mika Mwamba na kile kibao cha ‘JULLIETTA’ kilitoka na kumtambulisha vyema kwenye Medani ya Mziki.

Bila shaka ukimuuliza Mwanamuziki yeyote ambaye anatamba hivi sasa au ashawahi kutamba kuhusiana na hizi chati zetu za kibongo atakuambia ‘kuhiti  sio vigumu,vigumu ni kupakua hits baada ya hits’

Ujio wa Dully Sykes ulikuwa ni wa kipekee,bora na wa maana kabisa na cha kushangaza zaidi ni pale alipoongeza makakamavu na kuziacha sifa zimjenge badala ya kubweteka na ktk kulithibitisha hilo aliendelea kupakuwa mawe ya nguvu kama 1- stori ya ukweli 2- Nyambizi 3- Mr Misifa (alipewa na P Funk hilo jina) 4-Salome

Mwaka 2002 alizindua album yake ya kwanza pale Diamond Jubilee, na uzinduzi wake uliendeshwa kwa style ya NANI ZAIDI?kati yake na  T.i.d (Top in Dar) na mpaka tunarudi mitamboni ukumbi mzima ulikua upande wa Dully na hali hio haikunishangaza hata mimi kwasababu kazi za Dully zilikua sio kama zile za KOBE WA JUU YA MTI,yaani hapa namaanisha sio mpaka apandishwe ndo awe juu,so tayari mshajua nani alionekana kidume siku hiyo au vipi? Naomba tukumbuke ya kwamba style hii ya kuwapambanisha Magwiji hawa ilitumika kama njia ya kuwavutia mashabiki, kuwapa hamasa ili wajitokeze kwa wingi ukumbini na wala sio kama hawa jamaa walikua na Bifu kama ambavyo wengi walifikiri hapo mwanzoni au labda minong’ono ya nani mkali Mitaani.

Dully aliendelea kulitetea Taji hilo la Mkali wa Bongoflava kwa kupakuwa Mawe mengine ambayo yote yalihit au bado yanasumbua kwenye chati kama 1-Handsome  2-ladies free  3-kijakazi 4-hi  5-leah  6-tanita  7-Jackie  8-Eva  9- Rafiki  10-Latoya  11-Nakupenda 12-Ningejua 13-Mariah Mariah 14- Bijoux 15- hunifahamu 16-Loudspeaker 17-asha Mapromise 18-Baby Candy 19-Watasimuliwa 20-Miss Tz UK 21-Dhahabu 22- dully’s Chick 23-Kupenda 24-Malaika 25- Tamika 26-Opalina 27-Monalisa  28-Sikutaki tena  29-Papa 30-Tata 31-Shikide (ambayo inahit hivi sasa)

Uandishi wa nyimbo zake haupo kwa ajili ya kukufanya ufikirie sana ili kuelewa kile alichokiimba na uimbaji wake ni kama anafanya Mzaha hivi au unaweza sema hayuko serious lakini ukimtegea sikio zaidi utagundua nia na madhumuni yake ni kukufanya uburudike kwa kupitia sanaa yake na sanaa ni kitu ambacho hakina mipaka kama alivyosema Shaaban Robert, ni ukweli Dully Sykes anasifika kwa kuimba Nyimbo zenye ujumbe mwepesi na nyingi zikiwa ni za mapenzi au kujisifia yeye ni nani lakini ni nyimbo hizo hizo ndo zimemfanya akubalike na pia ninathubutu kusema ni aina ya Nyimbo ambazo Jamii inazielewa na kuzipandisha chati mapema zaidi kuliko zile za ki-u-wanaharakati.

VITUKO.

(1) Sote tunajua Chura anayapenda Maji lakini sio ya moto vivyo hivyo Dully anapenda sifa lakini isiwe na dharau ndani yake, moja kati ya matukio anayoyakumbuka ni pamoja na lile deni la shilingi mia moja ya kitanzania aliyokopeshwa na Mdau mmoja wa kitaani kwake kwa ahadi ya kuirudisha pindi tu akitoka au kufanikiwa kimziki… ‘unajua hakuna kitu cha bure sikuhizi,right?nakukopesha hii shing mia ya nauli leo, lakini naomba if utafanikiwa kimziki unirudishie shing mia yangu… ©Mdau

(deni hilo lilipwa tena kwa kiasi hicho hicho cha fedha miaka mitatu baadaye na hiyo ilitokana na yeye Dully kuwa bize na show nyingi za mikoani)

(2) Anasifika kwa kulamba lipsi zake na pia anahisi wasanii wengi wa bongo fleva wakiongozwa na Yule star wa mmarekani wakuitwa LL COOL J wanamgeza yeye Dully Sykes kulambalamba lipsi zake.

(3) Yeye ni mtu wa kwanza kuleta masuala ya Camp, (alipokuja na Misifaz Camp baada ya kuchoshwa na zile stunt za ZERO BRAIN) anajivunia kwa hilo na kwa upande mwingine anasikitika kwasababu ni Camp hiyo hiyo ndo iliyozaa na kulea asilimia kubwa ya Madansa na pia ni Misifaz Camp hiyo hiyo iliyosababisha watoto wa dogo watoboe masikio yao na kuyavika hereni au kujipiga tattoo kabla ya kuwauliza au kupewa ruhusa na wazazi wao, na pia ni Camp hiyohiyo iliyosababisha asilimia kubwa ya Madansa waashie shule za msingi au hata kufukuzwa wakiwa darasa la tatu na kuendelea.

(4) Msanii wa kwanza kupata Skendo mbaya Gazetini.

(5) Ana historia ya kuongea non stop toka mwanzo hadi mwisho wa safari, haijalishi umbali na pia ni Msanii ambaye anaiva na kila Msanii.

(6) Msanii pekee mwenye nyimbo nyingi zenye majina ya kike Duniani (kitabu cha Guinnes hakijamstukia tu)

OUTRO.

Dully ni mfano wa kuigwa mbele ya macho ya mbunifu yeyote sababu huwa haogopi kukosea na ambisheni zake ni  zakuongoza sio za ukifuata upepo… hafati ispokuwa anafatwa, na pia ana ujasiri wa kuzitetea hisia na hata kuwaprove wrong wale waliokuwa wanapinga style yake ya Muziki na  kuwanyamazisha wale wote waliokuwa wanampaka yeye ni Mwanasesere, Muuza sura tu au Mbana pua..

Wanamuita Mzazi wa Bongo Fleva kwasababu ni yeye ndie aliyeanzisha aina hii ya uimbaji ambao huwa una ladha ya kimwambao na zile za Bangra  kwa mbaali (na kama una sikio zuri utagundua kuna vionjo vya kicongo vimeongezwa  ili kutia Chachandu siku hizi) na amewainspaya WANABONGOFLAVA wengi na karibia wote wanalikubali hilo pasina kutaka mjadala au kuonyeshana uhodari wa maneno.

Dully anafurahia sana kuona WANABONGOFLAVA wapya wanavyofanikiwa kimaisha na pia anazikubali chalenji zao kwa moyo mweupe kabisa lakini anasema YEYE NI MKONGWE,KAMWE HATOKUBALI KUFUNZWA UTAMADUNI NA WATOTO.

Muziki kwake ni zaidi ya kipaji, yeye binafsi anaamini KIPAJI alichonacho ni kama ZAWADI aliyoshushiwa na Allah ili ajipatie rizki, anamaliza kwakusema ‘alijifunza yeye mwenyewe kupiga gitaa, keyboard na drumz,wala hakufundishwa na mtu yeyote’

Okay…. Baaaaaaaaaiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Download Some New Song

Posted: July 2, 2010 in Uncategorized
SUPPORT OUR LOCAL ARTISTS…BUY ORIGINAL ALBUMS>>>

Management of Radio Mbao is pleased to announce July 1st, 2010 is an official launch date of Radio Mbao (http://www.radiombao.com)

Our mission is to enlighten, excite, and educate people through our station’s program while offering a variety of music 24hrs a day.

In the meantime before July 1st, 2010, you can login to Radio Mbao website (http://www.radiombao.com) to listen to a variety of music 24hrs a day.

We will have different kind of live shows in our radio such as KOMBOLELA SHOW (hosted by Metty), REAL LIFE PROGRAM GOSPEL SHOW (Hosted by Amos), JIACHIE SHOW, ACT A FOOL SHOW etc. For more information about the programs and the radio, visit our website http://www.radiombao.com or contact us through info@radiombao.com, Michael@radiombao.com .

ADVERTISE WITH RADIO MBAO (BANNER + AUDIO ADS PACKAGE)

30 Ads every 24 hrs: 1 Week, $ 400.00

30 Ads every 24 hrs: 2 Weeks, $ 500.00

30 Ads every 24 hrs: 3 Weeks, $ 550.00

30 Ads every 24 hrs: 1 Month, $ 650.00

A two month campaign booked in advance would cost $ 1200.00.

All prices are based on Ads lasting a maximum of 45 seconds and these will be provided by the client on MP3 files. Banner and additional click-through links are included in the price and should be provided by the client in advance of the campaign.

Regards,

Michael Carter Mlingwa

www.radiombao.com

www.babkubwa.com

MZUNGU KICHAA Send off concert before the European tour. (His Tanzanian band Bongo Beat will be joining him in Denmark for the month of August). To mark and to celebrate this, we would like to invite you to the MZUNGU KICHAA SEND OFF CONCERT.

Click 2 Download The swagga Don

Intro
Fid Q: So Swagtastik!!!
Naj: Ngosha ze Swagga Don x4
Verse 1:
(Fid Q)
Mc’z wanaenda down, ka Zim(babwe) dollars/
Mie sio bling, mie culture ka ZEMKALA/
Da brightest thang shining next to a diaMOND/
Niite Ghost Writter ninapo Blaze ka AMO/
Mara nyingi mie nina bahati kama Lotto Machines/
Si mtu wa adventures kama Frodo kwenye Lord of the Rings/
Niite Roscoe, ninapoSPEAK in Tongues ka Jenkinz/
Don kama Bosco, Mad kama Ice Helsink/
Unataka Bed fight? Mie nina King size na French fries kwa Breakfast/ T- bone stake na PRISON BREAK kiGangstar/
Tattoo plan kama Michael Scolfield/
Bruce lee wa Rap ya Africa, Rock city naigeuza Rap City/
Nina Gucci Lips namaanisha ziko Brown/
Materialistic wanapenda niwe around/
Sexy & Single na pia hufurahi nikiwa FREE/
Nilipenda 3 sum zaidi ya unavyoipenda track hii/
Trust me, ninahitaji wife and some gorgeous Kids/
Seen, mie sio bogus we una dance ka Lotus juu ya hii beat/
Mashairi kwangu Pipi, nayagawa ka Santa Claus/
Kazi na Dawa Marco puff 3 kitu BOUNCE/
Mademu hawapendi kuona unavyomdiss FID/
Wote nawaita Candy sababu they’re so SWEET/
I’m so 2010 sihitaji Pad or Pen,u so 2000 and late/
Na haulipuki ka Bin Laden/

Chorus:
( Naj) Ngosha ze Swagga don x8
2nd Verse:
(Fid Q) My Mama.. didn’t raise no Fool/
Ninavyo Bust a Rhyme… wananiita Leader wa new School/
Ngosha ze SWAGGA DON.. Uh uh usinidownload/
Hapa utapata ladha expensive zaidi ya iPhone/
Mie sio Superstar ni International I con/
I’m Internationaly known kama Tyson/
Flow iko so Universal kama yvone, CHAKA CHAKA/
Ladies and Gentlemen ni Rappers Rapper hapa/
Naweza kwenda Quick kama ROCKA nikawatisha kisha mkaa ‘’ We Love you FIDQ’’ U deserve girls… Q yuko stronger ka playa wa Baseball au Wrestling/ usiniite Paper Chaser mie nina Chase Dreams/
Kama una Pesa Jenga kabla haujaanza Pimp Rimz/
Jikomboe kama wanaojiunga na X treme/
Drive with care, coz Life has no Spare/ na piiiiiiiiaaaaaaa…,.
‘’ THEY SAY IM COOL LIKE FIRE & AND IM HOT LIKE ICE OH UYEAH… U FEEL WHAT I SPEAK COZ I SPEAK WHAT I FEEL OH YEAH’ X2

SING IT!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Tamasha la Fiesta 2010 linakaribia kuanza,na kama ujuavyo tamasha hilo husheheni mambo kibao kwa wapenzi/washabiki wao.safari hii kwa mara ya kwanza tena linagonga hodi ndani ya mji kasoro bahari,Morogoro.Wakazi wa Morogoro Fiesta hiyo 2010 inawajia mkoani mwenu ikiwa na kauli mbiu yake JIPANGUSE Rrrrrrrhhhhhhaaaaa..! Huku Mdhamini mkuu wa tamasha hio ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka ni kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd.


Orodha ya wasaniii utakao Jipanguse nao ndio kama hao hapo juu,si hao tu na kuna wegineo kadhaa wa kadhaa akiwemo Mwana Fa,Amini na Linah kutoka THT.Kutakuwepo na michezo mbalimbali,Fiesta Jipanguse rrrhhhhhaaaaa 2010 itafanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri,July 7 kwa kiingilio cha sh 2000 kwa kila mmoja.Kama vile haitoshi July 9 tamasaha hilo litahamia mjini Arusha na kufanyika ndani ya Matongee .


Barua Ya sugu
napenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha wananchi wenzangu wa Mbeya Mjini, wapenzi wa muziki wangu, wanachama wenzangu wa CHADEMA na watanzania kwa ujumla tarehe 28 Juni 2010 nilikamatwa na polisi kwa kile walichonieleza kuwa kuna malalamiko dhidi yangu kuwa nimemtishia kwa maneno kumuua Ruge Mutahaba kupitia wimbo uitwao “Wanna Kill” uliopo kwenye album iitwayo “Anti Virus”.

Walinikamata saa 5 asubuhi nikiwa naingia ukumbi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya kutoa Mada kuhusu “Tathmini ya Muziki wa Kizazi Kipya na Hatma yake nchini” na kunihoji kwa takrabani masaa matano mpaka saa 10 jioni.

Wameniachia kwa kile walichonieleza kuwa ‘dhamana ya kujidhamini mwenyewe’ na kunitaka niripoti kwao siku ya jumatano tarehe 30 Juni saa 5 asubuhi siku ambayo nilipanga kwenye ratiba zangu kurejea nyumbani Mbeya Mjini kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kabla ya tarehe ya mwisho ya utoaji na upokeaji fomu ndani ya CHADEMA.

Katika mahojiano nao yaliyofanyika Makao Makuu ya Upelelezi Wizara ya Mambo ya Ndani; maofisa usalama (CID) walionihoji walirejea mstari mmoja katika kiitikio cha wimbo husika wenye maneno “I Wanna Kill Right Now” na kusema kwamba mlalamikaji ameutafsiri mstari huo kuwa ni tishio la kutaka kumuua.

Napenda kuwajulisha mashabiki wangu na watanzania wenzangu kwamba nimelieza wazi jeshi la polisi kwamba hakuna wimbo wala maneno niliyowahi kutamka kwa lengo la kukusudia kumuua binadamu yoyote. Niliwaeleza jeshi la polisi kwamba sanaa ya muziki inalugha zake zake za kifasihi.

Maadhui ya wimbo mzima yamejikita katika harakati zangu za siku zote za kupambana na wanyonyaji dhidi ya maslahi ya wasanii Tanzania na wimbo huo una maudhui ya kutaka “Kuondoa ama kuiua dhamira ya mbovu na nia zao ovu”.

Ni vyema mashabaki wangu, wanachama wenzangu na watanzania kwa ujumla wakarejea katika Kamusi mbalimbali za kimataifa ambapoo neno KILL linamaana zaidi ya 10 zikibeba pia maana ya KUKOMESHA, KUONDOA nk.

Katika wimbo huo nimeghani kwa kutumia fasihi mambo ya ukweli yanayotokea katika sekta ya sanaa na wala hauna dhamira yoyote wala maudhui ya kufanya kosa lolote la jinai; hivyo kama kuna mtu ameguswa na ukweli uliomo katika wimbo huo na hakubaliani nao basi aupinge kwa hoja ama akafungue madai badala ya kukimbilia kutaka kuliingiza jeshi la polisi kwenye masuala ya sanaa.

Aidha nimeshangazwa na hatua ya jalada hilo la polisi kufunguliwa ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Wizara ya Mambo ya Ndani yaliyopo Wilaya ya Ilala wakati mimi na mlalamikaji wote ni wakazi wa Wilaya ya Kinondoni.

Baada ya maelezo niliyoyatoa ni matumaini yangu kuwa jeshi la Polisi ambalo lina kazi muhimu zaidi ya kukabiliana na ujambazi na vitendo vingine vya uhalifu ambavyo vinazidi kuongezeka katika Mkoa wa Dar es salaam ambapo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yapo litaelekeza nguvu zake katika kukabiliana na vitendo hivyo vya makosa ya Jinai badala ya kupoteza muda wake kushughulikia masuala ya kifasihi ambayo yana sura ya madai yasiyo na uzito wowote.

Sikiliza Radio Mbao

Posted: July 2, 2010 in Uncategorized

CLICK 2 Listen

He goes by the name of Albino Fulani who recently organized an outstanding benefit concert to raise funds to help kids with albinism by providing sun blocks to prevent skin cancer who also participated in Baby Powder the movie has just released a HIT new single “NAFASI” Featuring Sugu and Belle 9 on chorus and Mwana FA on the 2nd verse. The song which was officially released at Friday night show on East Africa Television (EATV) song talks about things they will do if they were given a chance. Enjoy!!!!